Sunday, October 24, 2010

How to dress Appropriate for Work........!

Mara nyingi,siku za jumapili ikifika mida kama hii kila mtu anakuwa na mawazo 'kesho ntavaa nini kazini'' au kama ni 'chuo'au katika shughuli za kila siku za kutupatia kipato,sio wote wanaofikiria kuhusu hili..ila kwa mtu anaejipenda na anae penda kupendeza lazima ata come accross this problem..
Kuna baadhi ya ofisi wanavaa uniform kama Banks,or Hospitals and taasisi zingine but kwa wasiovaa uniform..nimejaribu kutafuta tips kwa akina dada or akina mama za jinsi ya vizuri kazini kwa kuwa simple,bila kutumia akili sana..
  • The Little Black Dress-sio lazima liwe black,bt rangi kama kijivu,light blue pia zinafaa kuvaa ofisini,lakini hakikisha ni gauni la heshima,lisibane sana,au kuonesha sehemu kubwa ya mwili.
  • Belt-chagua material yoyote uipendayo,uwe wa leather n.k,belts znasaidia kupendezesha kiuno..na kukufanya uvutie zaidi.
  • Accessories-epuka vikolombwezo vyenye nakshi nyingi,kama charm bracelets,au hereni kubwa ..
  • Shoes-jipende,tafuta viatu vizuri virefu bt sio virefu sana vikakufanya utake kuanguka au ushindwe kutembembea,lakin pia visiwe flat kabisa.labda kama una matatizo ya miguu na huwezi kuvaa viatu virefu,na kama utavaa viatu ambavyo vipo wazi kwenye vidole,hakikisha umesafisha kucha basi.
  • Scarf-faida kubwa ya scarf,if utachagua rangi nzuri ya scarf itanogesha vazi lako na pia kung'arisha uso.
  • Wear your size-usivae nguo ndogo sana au kubwa sana,vaa nguo znazoendana na mwili wako.

2 comments:

Rachel said...

Nimependa hii!! Poa sana

Anonymous said...

Ndiyo, labda kwa hivyo ni